Addis Ababa,Ethiopia.
MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Burundi aliyewahi kutamba nchini kwa nyakati tofauti akiwa na vilabu vya Yanga na Azam FC,Didier Kavumbagu,amejiunga na klabu ya EEPCO (Ethiopian Electric Power Corporation Football Club) inayoshiriki ligi kuu ya Ethiopia.
Kavumbagu amejiunga na EEPCO maarufu kama The Red Devils/Mashetani Wekundu baada ya mipango yake ya kucheza soka la kulipwa nchini Vietnam katika klabu ya Long Tam Long An kukwama kutokana na taratibu kadha kushindwa kukamilika.
EEPCO inayomilikwa na shirika la umeme la Ethiopia ina makao yake makuu katika mji mkuu wa Ethiopia,Addis Ababa na hutumia uwanja wa Mebrat Hail Stadium wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 8,000 kwa michezo yake ya nyumbani.
MAFANIKIO:NDANI YA MIPAKA
EEPCO imetwaa ubingwa wa ligi kuu ya Ethiopia (Ethiopian Premier League) mara tatu (3):1993, 1998, 2001
Ubingwa wa Kombe la Ligi (Ethiopian Cup) mara nne (4):1971, 1972, 1976, 2001
Ubingwa wa Super Cup (Ethiopian Super Cup) mara tatu (3):1993, 1998, 2001
MAFANIKIO:NJE YA MIPAKA- CAF
Ligi ya mabingwa Afrika (CAF Champions League) imeshiriki mara mbili (2)
1999 – Ilitolewa raundi ya kwanza
2002 – Ilitolewa katika hatua za awali (Preliminary Round)
0 comments:
Post a Comment