Shinyanga,Tanzania.
MABINGWA watetezi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara,Yanga SC,wameonja radha ya kufungwa msimu huu baada ya jioni ya leo kuchapwa bao 1-0 na Stand United katika mchezo mkali wa ligi hiyo uliochezwa katika uwanja wa CCM Kambarage,Shinyanga.
Mpaka mapumziko hakuna timu iliyokuwa imeuona wavu wa mwenzake licha ya kushambuliana mara kwa mara ambapo safu za ushambuliaji zilikosa utulivu wa kutumia nafasi zilizopatikana.
Kipindi cha pili Stand United ilifanikiwa kuibana vyema Yanga SC na kufanikiwa kupata bao pekee na la ushindi lililofungwa dakika ya 58 na Pastory Athanas baada ya kuwazidi ujanja walinzi Vincent Bossou na Vicent Andrew 'Dante' na kumfunga kirahisi Ally Mustafa Barthez.
Huo ni mchezo wa kwanza kwa Yanga SC kupoteza tangu msimu mpya wa 2016/17 uliopoanza.
0 comments:
Post a Comment