Dar Es Salaam,Tanzania.
Mechi mbili za raundi ya sita za Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Majimaji, na African Lyon na Kagera Sugar sasa zitachezwa kwenye Uwanja wa Taifa badala ya Uwanja wa Uhuru.
Mabadiliko hayo yametokana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kusitisha kwa muda kuutumia Uwanja wa Uhuru katika kipindi hiki ambacho limeanza kufanyia marekebisho sehemu ya uwanja huo ambayo ni ya nyasi bandia (artificial turf).
Hivyo, mechi ya Simba na Majimaji itafanyika Jumamosi, Septemba 24 wakati ile ya African Lyon na Kagera Sugar itachezwa Jumatatu,Septemba 26.
Jumapili, Septemba 25 Uwanja Taifa utatumiwa kwa mechi ya timu za Wabunge za Simba na Yanga ili kuchangia waathirika wa janga la tetemeko lililotokea mkoani Kagera.
Mechi nyingine za Ligi Kuu ya Vodacom zitakazochezwa Jumamosi, Septemba 24 ni kati ya JKT Ruvu na Mbeya City (Mabatini),Ndanda na Azam (Nangwanda Sijaona),Tanzania Prisons na Mwadui (Sokoine),Mtibwa Sugar na Mbao (Manungu).
Jumapili kutakuwa na mechi kati ya Stand United na Yanga (Kambarage), na Ruvu Shooting na Toto Africans kwenye Uwanja wa Mlandizi mkoani Pwani.
Kutokana na marekebisho yanayofanyika Uwanja wa Uhuru, mechi ya kundi ya A ya Ligi Daraja la Kwanza kati ya AshantiUnited na Pamba iliyokuwa ichezwe Ijumaa,Septemba 23 kwenye uwanja huo sasa itafanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment