London, Uingereza.
UKIACHANA na ushindi mnono wa mabao 2-0 iliyoupata nyumbani dhidi ya FC Basel kwenye mchezo wake wa kundi A wa michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya hamu kubwa kwa mashabiki wengi wa soka imekuwa ni kutaka kujua kwanini Arsenal walivaa jezi za ugenini wakati wao ndiyo walikuwa wenyeji wa mtanange huo??
Jibu ni kwamba Arsenal walilazimika kuvaa jezi za ugenini,njano, badala ya jezi zao za nyumbani ,nyekundu, hii ni baada ya jezi hizo kushabihiana kwa karibu na jezi za FC Basel ambazo ni nyeupe,blue na nyekundu.
Hivyo baada ya kushabihiana huko kwa jezi na FC Basel kutokuwa na jezi ya tatu yaani third kit,UEFA,iliitaka Arsenal kuachana na jezi zake za nyumbani na kuvaaa za ugenini.
Hii ni mara ya tatu sasa Arsenal inalazimika kutumia jezi za ugenini ikiwa nyumbani katika michezo ya ligi ya mabingwa Ulaya.Mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 1991ilipovaana na Benfica ya Ureno.Mara ya pili ilikuwa ni mwaka 1999 ilipocheza dhidi ya Lens ya Ufaransa.
Ikumbukwe kanuni ya mwaka 1998/99 ya michuano ya UEFA inaagiza iwapo kutatokea kushabihiana/kufanana kwa jezi chaguo la kwanza basi timu mwenyeji italazimika kubadili jezi.
0 comments:
Post a Comment