728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, September 27, 2016

    EPL:WAGENI BURNLEY WAWATOA NISHAI WABISHI WATFORD WAWAGONGA 2-0 TURF MOOR


    Burnley,Uingereza.

    LIGI KUU ya England maarufu kama EPL iliendelea tena Jumatatu usiku kwa mchezo mmoja kuchezwa katika dimba la uwanja wa Turf Moor ambapo wageni katika ligi hiyo Burnley walikuwa nyumbani kupepetana na watukutu Watford mbele ya watazamaji 18519.

    Mpaka mapumziko wenyeji Burnley walikuwa mbele kwa bao moja lililofungwa dakika ya 38 na Jeff Hendrick kwa kichwa akitumia vyema pasi safi ya kiungo Mbelgiji, Steven Defour. 

    Kipindi cha pili kilikuwa kizuri kwa mara nyingine kwa Burnley kwani dakika tano baada ya kuanza kwa kipindi hicho yaani dakika ya 50 walifanikiwa kupata bao la pili lililofungwa kwa kichwa na mlinzi Michael Keane.

    Keane alifunga bao hilo akiunganisha krosi safi ya kiungo Steven Defour ambaye alikuwa mwiba mchungu katika mchezo huo.Ushindi huo umeinyanyua Burnley mpaka nafasi ya 13 baada ya kufikisha pointi saba huku Watford ikibaki nafasi ya 11 na pointi zake saba pia.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: EPL:WAGENI BURNLEY WAWATOA NISHAI WABISHI WATFORD WAWAGONGA 2-0 TURF MOOR Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top