Manchester, Uingereza.
KIUNGO wa Manchester City,Yaya Toure,amestaafu kuichezea timu yake ya taifa ya Ivory Coast maarufu kama Tembo wa Afrika Magharibi.
Toure mwenye umri wa miaka 33 sasa ametangaza uwamuzi huo muda mfupi uliopita na kuhitimisha huduma yake ya miaka 14 ya kuitumikia Ivory Coast.
Toure mshindi mara nne mfululizo wa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika anaiacha Ivory Coast akiwa ameichezea michezo 113 huku mwaka 2015 akiisaidia kutwaa ubingwa wa mataifa huru Afrika maarufu kama AFCON.
0 comments:
Post a Comment