Dar Es Salaam,Tanzania.
MWENYEKITI wa Yanga SC,
Yussuf Manji ameipa klabu hiyo kongwe nchini eneo la Ekari 715 ufukweni mwa Bahari ya Hindi, upande wa Geza Ulole, Kigamboni, Dar Es Salaam.
Wasaidizi wa Manji wamekabidhi eneo hilo leo mchana katika hafla fupi iliyohudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Ndani,Mwigulu Nchemba na Maofisa wa chama na Serikali ya Kigamboni.
Aliyepokea eneo hilo kwa niaba ya klabu ni Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa klabu,Mama Fatma Karume aliyeambatana na Mjumbe mwingine wa Bodi hiyo, Dk Jabir Idris Katundu,Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu, Samuel Lukumay na Katibu Mkuu, Baraka Deusdedit.
0 comments:
Post a Comment