Paris,Ufaransa.
WAFARANSA hawataki ujinga safari hii.Wanaitaka mapema tiketi ya kuwemo kwenye michuano ya kombe la dunia la mwaka 2018 huko nchini Urusi na katika kuonyesha kuwa hawatanii katika hilo wamemtosa mshambuliaji anayesugua benchi kwa sasa Arsenal,Olivier Giroud.
Giroud hajajumuishwa kikosini kwa sababu kubwa mbili.Mosi msimu huu hajaanza mchezo hata mmoja akiwa kikosi cha kwanza cha Arsenal.Pili amekuwa na maumivu ya dole gumba la mguu wake wa kushoto ambao ndio mguu wake wa kufanyia kazi.
Mwingine aliyefungiwa vioo katika uteuzi huo ni mshambuliaji wa Real Madrid,Karim Benzema.Benzema hajaitwa kwa kuwa bado ana kesi ya kujibu katika tuhumu za ulaghai dhidi nyota mwenzie wa Ufaransa, Mathieu Valbuena.
Wakati Giroud na Benzema wakitoswa,beki wa Athletic Bilbao,Aymeric Laporte,amejumuishwa kwa mara ya kwanza kikosini na kocha Didier Deschamps katika kikosi kitakachovaana na Bulgaria pamoja na Uholanzi mwezi Octoba kuwania tiketi ya kufuzu kombe la dunia.
Wengine waliojumuishwa kwenye kikosi hicho ni nyota wa Manchester United,Paul Pogba na Anthony Martial.Moussa Sissoko na Hugo Lloris wa Tottenham.Laurent Koscielny wa Arsenal,N'Golo Kante wa Chelsea, Bacary Sagna wa Manchester City na Dimitri
Payet wa Westham United.
Nyota wa Crystal Palace,Yohan Cabaye na Steve Mandanda nao wamejumuishwa.
KIKOSI KAMILI
Makipa: Alphonse Areola (PSG), Hugo Lloris (Tottenham), Steve Mandanda (Crystal Palace)
Mabeki:Lucas Digne (Barcelona),Laurent Koscielny (Arsenal), Layvin
Kurzawa (PSG), Aymeric Laporte (Athletic Bilbao), Jeremy Mathieu (Barcelona),Bacary Sagna (Manchester City), Djibril Sidibe (Monaco), Raphael Varane (Real Madrid)
Viungo:Yohan Cabaye (Crystal Palace),N'Golo Kante (Chelsea), Blaise Matuidi (PSG), Dimitri Payet (West Ham), Paul Pogba (Manchester United), Moussa Sissoko (Tottenham)
Washambuliaji:Kingsley Coman (Bayern Munich),Nabil Fekir (Lyon), Kevin Gameiro (Atletico Madrid), Andre-Pierre Gignac (Tigres UANL),Antoine Griezmann (Atletico Madrid),Anthony Martial (Manchester United)
0 comments:
Post a Comment