728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, September 22, 2016

    SERGIO BUSQUETS AAMUA KUZEEKEA BARCELONA


    Barcelona, Hispania.

    SERGIO Busquets ameamua kuzeekea Barcelona hii ni baada ya leo jioni kusaini kandarasi mpya ya miaka mitano ya kuendelea kuwatumikia mabingwa hao watetezi wa ligi ya La Liga.

    Kandarasi hiyo mpya itamfanya Busquets,28, aendelee kuwa mali ya Barcelona mpaka mwaka 2021 huku pia ikimpa nafasi ya kuongeza miaka miwili zaidi ambayo itamfanya aendelee kubaki Nou Camp mpaka mwaka 2023.

    Aidha kandarasi hiyo mpya pia imebeba kipengele ambacho kitatoa nafasi kwa Busquets kuihama Barcelona kwa ada ya uhamisho ya €200m.

    Busquets alianza kuichezea Barcelona mwaka 2008 wakati huo ikiwa chini ya kocha Pep Guardiola.Mpaka sasa amefanikiwa kuichezea Barcelona jumla ya michezo 390 akifunga mabao 12 na kutwaa mataji lukuki.

    Mataji hayo ni:Klabu bingwa Ulaya mara tatu.Mataji sita ya La Liga,Mataji manne ya Copa del Rey,Mataji matatu ya kombe la dunia la vilabu.Mataji matano ya Spanish Super Cup.

     


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SERGIO BUSQUETS AAMUA KUZEEKEA BARCELONA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top