Dar Es Salaam,Tanzania.
LIGI KUU ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) itaendelea tena leo Jumapili Septemba 25,2016 kwa michezo miwili kuchezwa katika miji ya Shinyanga na Mlandizi,Pwani.
Mabingwa watetezi wa ligi hiyo,Dar Young Africans,watakuwa watakuwa mjini Shinyanga katika uwanja wa CCM Kambarage kuvaana na wenyeji wao Stand United katika mchezo unaotarajiwa kuwa utakuwa mkali na wa kusisimua.
Maafande wa Ruvu Shooting wao watakuwa nyumbani kwao katika uwanja wa Mabatini, huko Mlandizi,Pwani kucheza na Toto Africans ya Mwanza.
Ligi hiyo itaendelea tena kesho Jumatatu kwa mchezo mmoja kuchezwa katika Uwanja wa Taifa,Dar Es Salaam,ambapo African Lyon watamenyana na Kagera Sugar ya mkoani Kagera.
0 comments:
Post a Comment