Rabat,Morocco.
MO BEJAIA imeungana na miamba wa Congo DR,TP Mazembe,kufuzu fainali ya michuano ya kombe la shirikisho Afrika baada ya Jumapili Usiku kubebwa na faida ya bao la ugenini kufuatia kupata sare ya bao 1-1 na FUS Rabat ya Morocco katika mchezo wa pili wa nusu fainali uliopigwa katika uwanja wa Complexe sportif Prince Moulay-Abdallah,Rabat.
Wenyeji FUS Rabat ndiyo walitangulia kufunga dakika ya 74 kwa bao la Mohammed Nahiri na MO Bejaia wakasawazisha dakika ya 90 kwa bao la Faouzi Rahal.
Ikumbukwe katika mchezo wa awali uliochezwa huko Bejaia wikendi iliyopita timu hizo zilishindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya 0-0 hivyo sare ya 1-1 imeipa ushindi Mo Bejaia.
Sasa TP Mazembe na MO Bejaia zitacheza fainali itakayokuwa ya mikondo miwili ya nyumbani na ugenini.Fainali hizo mbili zitachezwa kati ya Oktoba 28-30 kwa Mechi ya Kwanza na Marudiano ni kati ya Novemba 4-6.
0 comments:
Post a Comment