728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, September 26, 2016

    LIGI KUU BARA:KAGERA SUGAR YAINYUKA AFRICAN LYON 2-0 U/TAIFA


    Dar Es Salaam,Tanzania.

    LIGI KUU ya Vodacom Tanzania Bara maarufu kama VPL imeendelea tena jioni ya leo kwa mchezo mmoja kuchezwa katika dimba la Uwanja wa Taifa,jijini Dar Es Salaam ambapo African Lyon walikuwa wenyeji wa Kagera Sugar toka Mkoani Kagera.

    Mpaka dakika tisini za mchezo huo zinakamilika,wageni Kagera Sugar, ndiyo waliofanikiwa kujinyakulia pointi zote tatu baada ya kuwachapa wenyeji wao African Lyon kwa mabao 2-0.

    Danny Mrwanda alianza kuifungia Kagera Sugar bao la kuongoza 38 ya kipindi cha kwanza kabla ya Seleman kuongeza la pili dakika ya 40.

    Ushindi huo umeipeleka Kagera Sugar mpaka nafasi ya sita ya msimamo wa ligi baada ya kujikusanyia pointi tisa katika michezo sita.African Lyon imebaki nafasi ya kumi na moja na pointi zake sita.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: LIGI KUU BARA:KAGERA SUGAR YAINYUKA AFRICAN LYON 2-0 U/TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top