728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, September 22, 2016

    MESSI AUMIA BARCA IKILAZIMISHWA SARE NYUMBANI NA ATLETICO MADRID,


    Barcelona, Hispania.

    BARCELONA imeshindwa kupunguza tofauti ya pointi kati yake na vinara Real Madrid baada ya usiku huu kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Atletico Madrid katika mchezo mkali wa ligi ya La Liga uliochezwa katika uwanja wa Camp Nou,Barcelona.

    Ivan Rakitic aliifungia Barcelona bao la kuongoza kwa kichwa dakika ya 41 ya kipindi cha kwanza na kufanya Barcelona iende mapumziko ikiwa mbele kwa bao hilo moja.

    Kipindi cha pili kilikuwa kizuri kwa Atletico Madrid kwani walifanikiwa kuibana vyema Barcelona na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha dakika ya dakika ya 67 kupitia kwa Angel Correa.

    Aidha katika mchezo huo Barcelona ilipata pigo baada ya nahodha wake Lionel Messi kushindwa kumaliza mchezo baada ya kuumia.

     



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MESSI AUMIA BARCA IKILAZIMISHWA SARE NYUMBANI NA ATLETICO MADRID, Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top