Paris,Ufaransa.
BEKI wa Paris Saint-Germain,Muivory Coast,Serge Aurier,amehukumiwa kwenda jela kwa kipindi cha miezi miwili baada ya kukutwa na hatia ya kumshambulia Ofisa mmoja wa Polisi.
Hata hivyo Aurier mwenye miaka 23 hatatumikia kifungo hicho jela na badala yake atatumikia kifungo hicho akiwa nje kwa kufanya kazi/shughuri mbalimbali za kijamii.
Mbali na adhabu hiyo Aurier pia ametakiwa kulipa faini ya Paundi 521 (Tsh 1303500) pamoja na kulipia gharama za kesi/mahakama zinazofikia Paundi 1,300 (Tsh 3250000).
Mei 30 mwaka huu Aurier akiwa katika klabu mmoja ya usiku jijini Paris alijikuta akiingia matatani baada ya kuwatukana na kisha kumchapa kiwiko Ofisa wa mmoja wa Polisi wakati akitakiwa kutoa maelezo baada ya kubainika kuwa alikuwa amepaki vibaya gari lake aina ya Porsche Cayenne huku akihisiwa kuwa alikuwa amelewa.
0 comments:
Post a Comment