London,Uingereza.
WESTHAM United imeendelea kuandamwa na bahati mbaya ya kutopata ushindi tangu ilipohamia katika uwanja wake mpya wa London Stadium hii ni baada ya leo jioni kuchabangwa mabao 3-0 na Southampton katika mchezo pekee wa ligi kuu England uliochezwa Jumapili ya leo.
Mabao yaliyoendelea kuleta simanzi mioyoni mwa mashabiki wa Westham United yamefungwa dakika za 40, 62 na 92 na Dusan Tadic na Charlie Austin, James Ward-Prowse.
Kipigo hicho kimekuwa cha tano kwa Westham United katika michezo sita iliyopita ya ligi kuu England msimu huu na imekaa nafasi ya kumi na nane katika msimamo.Southampton imepanda mpaka nafasi ya nne.
0 comments:
Post a Comment