728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, September 27, 2016

    NAHODHA WESTHAM ASEMA UWANJA MPYA NDIYO SABABU YA WAO KUFANYA VIBAYA ENGLAND


    Na.Fredy Matic! 

    London,England.

    KIUNGO na nahodha wa Westham United,Mwingereza,Mark Noble,amesema kuwa kuhama kwenye uwanja wao wa zamani wa Upton Park kwenda kwenye uwanja wao mpya wa London Stadium ni miongoni mwa sababu zilizofanya timu yao ishindwe kufanya vizuri msimu huu.

    Westham United ambayo ipo chini kwenye timu tatu za chini wakiwepo Sunderland na Stoke City haijawa na msimu mzuri chini ya kocha wao Slaven Billic! Kwani katika michezo minne iliyopita imeruhusu kufungwa mabao 14 mpaka sasa.

    Licha ya kuandamwa na balaa la majeruhi wengi kwenye kikosi chao lakini Noble hajasita kuamini kuwa kuhama kwenye uwanja wao wa zamani wa Upton Park kumeiathiri kwa kiasi kikubwa sana klabu hiyo.




    Amesema "Kipindi tupo Upton Park tulikuwa na uwezo wa kukusanya pointi 20 nyumbani lakini hali imekuwa tofauti katika huu uwanja wa London Olympiki Stadium na kuongeza kuwa hata ile hali ya kujiamini kwa wachezaji imetoweka.

    Msimu huu Westham United haijawa na mwenendo mzuri kwani katika mechi sita za ligi kuu imepoteza michezo mitano na kushinda mchezo moja pekee huku wakipoteza michezo minne kwenye uwanja wao mpya.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: NAHODHA WESTHAM ASEMA UWANJA MPYA NDIYO SABABU YA WAO KUFANYA VIBAYA ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top