Lubumbashi,Congo DR.
MIAMBA wa Congo DR,TP Mazembe wanayochezewa na Mtanzania,Thomas Ulimwengu,wamefanikiwa kufuzu fainali ya michuano ya kombe la shirikisho Afrika baada ya jioni ya leo kutoka sare ya bila kufungana na miamba wa Tunisia,Etoile du Sahel,katika mchezo mkali wa nusu fainali ya pili wa michuano hiyo uliochezwa katika uwanja wa Stade Frederic Kibassa Maliba, Lubumbashi.
Kufuatia sare hiyo ya bila kufungana,TP Mazembe,imefaidika na bao la ugenini kwani katika mchezo wa awali uliochezwa wiki iliyopita mjini Sousse,Tunisia matokeo yalikuwa 1-1.
Etoile du Sahel ilipata bao lake kupitia kwa Hamza Lahmar huku TP Mazembe ikisawazisha kupitia kwa Roger Assale.
TP Mazembe sasa inasubiri mshindi kati ya MO Bejaia ya Algeria na FUS Rabat ya Morocco ambao watavaana leo usiku katika nusu fainali ya pili.
Fainali itachezwa katika awamu mbili.Awamu ya kwanza itakuwa kati ya Octoba 28 na 30 huku awamu ya pili ikiwa katika ya Novembe 4 na 6.
0 comments:
Post a Comment