728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, September 29, 2016

    MKWASA ATAJA 24 WA KUIVAA ETHIOPIA,KIPAO APETA TENA


    Dar Es Salaam,Tanzania.

    Kocha Mkuu wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania (Taifa Stars), Charles Boniface Mkwasa ametaja majina ya nyota 24 watakaounda kikosi ambacho kitasafiri mwishoni mwa wiki ijayo kwenda Addis Ababa, Ethiopia kucheza na wenyeji wetu kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika Oktoba 8, mwaka huu.

    Mkwasa maarufu kwa jina la Master amesema wachezaji aliowaita wataingia kambini Oktoba 2, 2016 kabla ya kuanza kukiandaa kuanzia Oktoba 3, 2016 ikiwa mara baada ya michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara ya mwishoni mwa wiki hii ambako Mwadui itacheza na Azam huku Mbao ikishindina na JKT Ruvu Oktoba 2, mwaka huu.

    Nyota wa Stars walioitwa na Mkwasa ni:

    Makipa

    Deogratius Munishi – Young Africans

    Said Kipao – JKT Ruvu

    Aishi Manula – Azam FC

    Mabeki

    Shomari Kapombe – Azam FC

    Juma Abdul – Young Africans

    Vicent Andrew - Young Africans

    Mwinyi Haji - Young Africans

    Mohamed Hussein – Simba SC

    David Mwantika - Azam FC

    James Josephat – Tanzania Prisons

    Viungo wa Kati

    Himid Mao - Azam FC

    Mohammed Ibrahim – Simba SC

    Jonas Mkude – Simba SC

    Muzamiru Yassin – Simba SC

    Viungo wa Pembeni

    Shiza Kichuya – Simba SC

    Simon Msuva - Young Africans

    Juma Mahadhi - Young Africans

    Jamal Mnyate – Simba

    Hassan Kabunda – Mwadui FC

    Washambuliaji

    Ibrahim Ajib – Simba SC

    John Bocco - Azam FC

    Mbwana Samatta - CK Genk ya Ubelgiji

    Elius Maguli – Oman

    Thomas Ulimwengu – TP Mazembe Congo.

    Mchezo huo utakaofanyika jijini Addis Ababa,umeratibiwa kwa mujibu wa kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ambalo huwa na kalenda ya wiki ya mechi za kimataifa kwa wanachama wake –Tanzania ni miongoni mwao. 

    Hii ni faida kwa Tanzania kama itashinda mchezo huo kwa maana kina alama za nyongeza kama inatokea unaifunga timu mwenyeji.

    Matokeo ya mchezo huo, ni sehemu malumu kupima viwango vya ubora na uwezo wa timu za taifa.

    Kwa sasa Tanzania inashika nafasi ya 132 kati ya nchi 205 wanachama wa FIFA zilizopimwa ubora. Ethiopia yenyewe inashika nafasi ya 126.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MKWASA ATAJA 24 WA KUIVAA ETHIOPIA,KIPAO APETA TENA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top