728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, September 28, 2016

    MWANASOKA AKAMATWA NA KETE 22 ZA DAWA ZA KULEVYA


    Port Louis,Mauritius.

    MLINDA MLANGO wa kimataifa wa Mauritius,Joseph Kinsley Steward Leopold,ametiwa nguvuni na wanausalama wa nchi hiyo baada ya kukutwa na madawa ya kulevya.

    Habari kutoka Mauritius zinasema Leopold mwenye umri wa miaka 27 alitiwa nguvuni Jana Jumanne baada ya maafisa wa idara ya kupambana na biashara haramu ya dawa za kulevya kufanya msako wa kushtukiza nyumbani kwake huko Port Louis na kumkuta na kete 22 za madawa ya kulevya aina ya heroin.

    Mbali ya madawa hayo pia Leopold amekutwa na vifaa vinavyodhaniwa kuwa vilikuwa vikitumia katika kuandalia na kuhifadhia dawa hizo haramu.Vifaa hivyo ni viwembe (Nyembe) na mzani mdogo.

    Leopold ni mlinda mlango namba moja wa klabu ya ASPL 2000 inayoshiriki ligi kuu ya Mauritius maarufu kama Mauritius Professional Football League na ni mlinda mlango chaguo la pili katika timu yake ya taifa ya Mauritius.

    Taarifa za ndani kutoka kwa wanausalama wa Mauritius zinasema Leopold ametiwa nguvuni baada ya jeshi la polisi kumfuatilia kwa kipindi kirefu pasipo mwenyewe kugundua.




    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MWANASOKA AKAMATWA NA KETE 22 ZA DAWA ZA KULEVYA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top