Casablanca,Morocco.
ZAMALEK imeungana na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kutinga fainali ya ligi ya mabingwa Afrika licha ya Jumamosi usiku kuchabangwa mabao 5-2 na Wydad Casablanca katika mchezo wa pili wa nusu fainali uliochezwa huko Rabat,Morocco.
Wydad Casablanca walijipatia mabao yao kupitia kwa William Jebor aliyefunga mara mbili, Ismail El Haddad Fabrice na N'Guessi Ondama huku yale ya Zamalek yakifungwa na Bassin Morsi na Stanley Nka Ohawuchi.
Matokeo hayo yameifanya Zamalek ifuzu fainali kwa jumla ya mabao 6-5 hii ni baada ya kushinda mchezo wa awali kwa mabao 4-0 huko Alexandria wiki moja iliyopita.
Fainali ya kwanza itachezwa kati ya Octoba 14-16 na ile ya pili itachezwa kati ya Octoba 21-23 na bingwa atajinyakulia zawadi ya dola za Marekani milioni 1.5 pamoja na tiketi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa ya dunia huko Japan mwezi Disemba.
0 comments:
Post a Comment