Dar Es Salaam,Tanzania.
NAHODHA na kiungo wa Simba SC Jonas Mkude amedai kuwa baada ya kuifunga Azam akili na mawazo yao kwa sasa ni katika mechi dhidi ya watani zao wa jadi Yanga na kama watashinda mchezo huo atakuwa na uhakika wa ubingwa msimu huu.
Mkude amesema, Yanga kwa sasa ndiyo timu pekee inayowaumiza kichwa na lengo lao ni kulipa kisasi cha kufungwa mechi zote mbili za msimu uliopita.
“Tuna mchezo Jumamosi na Majimaji FC, lakini huo ni mchezo wa kawaida kwetu kwa sababu ni timu nyepesi na tayari imeshapoteza michezo mitano ya awali. Mtihani wetu upo kwa Yanga watani zetu ambao ushindi pekee ndiyo utanogesha ubingwa wetu msimu huu,” alisema Mkude.
Mchezo baina ya Yanga na Simba utapigwa Oktoba 1 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Hadi sasa Simba ndiyo vinara wa kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ikiwa na pointi 13 huku Yanga wakishika nafasi ya pili wakiwa na pointi 10 lakini wakicheza mechi pungufu.
0 comments:
Post a Comment