Nice,Ufaransa.
MARIO Balotelli ameendeleza rekodi yake nzuri ya kupachika mabao muhimu tangu alipotua ligi daraja la kwanza Ufaransa maarufu kama Ligue 1 baada ya Jumatano usiku kufunga mabao mawili na kuiwezesha Nice kuchomoza na ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Monacco.
Balotelli alifunga mabao hayo mawili moja katika kila kipindi na kuipeleka Nice mpaka kileleni mwa msimamo wa ligi.Mabao hayo yamemfanya Bakotelli kufikisha mabao manne katika michezo miwili.
Mabao mengine ya Nice yamefungwa na Paul Baysse aliyefunga bao la kwanza na Alassane Plea aliyefunga bao la nne.
Aidha katika mchezo huo straika wa zamani wa Manchester United na Chelsea, Radamel Falcao Garcia,alilazimika kukimbizwa hospitali baada ya kugongana vibaya na kipa wa Nice.
Katika mchezo mwingine wa Ligue 1:Bordeaux imeifunga Metz mabao 3-0.Mabao yamefungwa na Malcom,Gaetan Laborde na Kiese Thelin.
Lyon imetoka nyuma na kuichapa mtu 10 Montpellier kwa mabao 5-1 yaliyofungwa na Nabil Fekir na Corentin Tolisso waliofunga mara mbili kila mmoja.Bao la Montpellier limefungwa na Morgan Sanson.
0 comments:
Post a Comment