Baada ya klabu ya Arsenal kukumbwa na balaa la majeruhi
katika kikosi chake na kuwapoteza walinzi Mathieu Debuchy na Nacho Monreal huku kukiwa na hatihati pia
ya kukosa huduma ya mlinzi wake kinda Calum Chambers katika mchezo wa leo wa
ligi ya mabingwa dhidi ya Dortmund kutokana na kuwa majeruhi kuna jipya
limeibuka klabuni hapo.
Usajili umefungwa wiki mbili zilizopita,Arsenal imebaki na
walinzi watatu pekee wa kujaza nafasi nne za safu hiyo.Je,unajua kinachotaka
kufanyika?
Habari zisizo rasmi sana zinasema klabu ya Arsenal imeanza
mawindo ya kuhakikisha inafanya usajili wa muda mfupi (miezi 3) ili kuziba pengo lililopo katika nafasi ya ulinzi hasa
kulia.Baadhi ya majina yanayotajwa tajwa ni haya yafuatayo.
1. Antony Reveillere (34)
Huyo ni mlinzi wa zamani wa vilabu
vya Lyon,Rennes.Aliichezea Ufaransa katika fainali za kombe la dunia mwaka 2010
pamoja na Euro 2012.
2. George McCartney (33)
Nyota wa zamani wa vilabu vya
Sunderland na Westham.Alitemwa na Westham msimu uliopita baada ya kuichezea
klabu hiyo michezo 20.Mmoja kati ya walinzi wazoefu wa Epl.
3. Oguchi Onyewu (32)
Nyota wa zamani wa vilabu vya Metz,Ac
Milan,Newcastle,Qpr na Shelfield Wednesday
0 comments:
Post a Comment