Habari na Paul Manjale
0717 70 55 48
Ikiwa hata wiki moja haijaisha tangu dirisha la usajili
lifungwe nchini England na sehemu nyingine duniani kocha wa klabu ya Arsenal
Mfaransa Arsene Wenger ameendelea na harakati za kukiimarisha kikosi chake ili
kiweze kufanya vizuri katika michuano yake mbalimbali ya ndani na nnje.
Akiwa amegungua mapema kuwa kosa la kutosajili walinzi wa
kutosha litamletea balaa mbele ya safari tayari kocha huyo ameanza kumfukuzia
mlinzi mkongwe na nahodha wa timu ya taifa ya Colombia Mario Yepez mwenye umri
wa miaka 38.
Mario Yepez ambaye kwa sasa ni mchezaji huru baada ya
kuachwa na klabu yake ya zamani ya Atalanta na Ac Milan vinayoshiriki ligi ya Seria A ya
Italia aliiongoza timu yake ya taifa ya Colombia kufika robo fainali ya kombe
la dunia nchini Brazil na kutolewa na wenyeji kwa magoli 2-1.
Habari kutoka vyazo mbalimbali zinasema Arsene Wenger
anataka kumpa nyota huyo mkongwe mkataba wa mwaka mmoja ili kuimarisha safu
yake ya ulinzi wa kati iliyo chini ya Laurent Koscienly,Per Mertesacker na
kinda Calum Chambers.
Kuja
kwa Yepez Arsenal kutamfanya nyota huyo kufikisha miaka 14 ya kucheza soka
barani Ulaya huku 10 mingine akiitumia kucheza barani Amerika ya kusini
Colombia na kwingineko
0 comments:
Post a Comment