Kocha mkuu wa klabu ya
Liverpool Brendan Rodgers amemwagia sifa lukuki nyota wake Mario Balotelli
kufuatia mwenendo mzuri anaoendelea kuuonyesha nje na ndani ya uwanja hasa
katika mchezo wa jumamosi dhidi ya Everton.
Rodgers amesifia mwenendo huo
hasa baada ya nyota huyo kuonekana mtulivu licha ya kufanyiwa madhambi ya mara
kwa mara na wachezaji wa Everton yaliyokuwa na lengo la kumkera ili achukie na
kulipiza.Akifanya mahojiano
baada ya mchezo huo Rodgers amesema
baada ya mchezo huo Rodgers amesema
“Anahitaji
kuweka akili yake mchezoni kila mara na hilo nilimwambia mapema tu.Hii ni mechi
ambayo joto lake huwa liko juu sana na huwa ngumu.Kiujumla alicheza vizuri
mchezo huo ukianzia kujituma mpaka nidhamu yake vyote vilikuwa sawia,vilivutia
na ilionekana kama angefunga goli.Nimehuzunika kwakuwa hakupata bahati ya
kufunga lakini kama ataendelea hivi magoli hayako mbali atafunga tu.Tangu atue
hapa amekuwa akiendelea vizuri,vizuri sana.Alimaliza kocha huyo kumwagia sifa
nyota huyo ambaye bado hajafanikiwa kufunga bao lolote katika ligi ya Epl.
Balotelli akikunjana na aliyekuwa kocha wake Roberto Manchini |
0 comments:
Post a Comment