Mitanange ya kuwania tiketi ya kufuzu michuano ijayo ya Ulaya
(Euro 2016) iliendelea usiku wa jana kwa miamba kadhaa ya soka barani humo
kushuka viwanjani kuwania pointi tatu muhimu.Baadhi ya matokeo ya mitanange
hiyo ni kama ifuatavyo……
GROUP A:
Timu ya taifa ya Uholanzi ikiongozwa kwa mara ya kwanza na
kocha wake mpya Guus Hiddink ilijikuta ikiangukia pua baada ya kukubali kichapo
cha bao 2-1 toka kwa wenyeji Jamhuri ya Czech katika mtanange uliopigwa mjini
Prague.
Mlinzi Janmaat akisikitika baada ya kufungisha goli |
Wenyeji Czech wakipata nguvu toka kwa mashabiki wao walikuwa
wa kwanza kupata bao kipindi cha kwanza kupitia kwa mchezaji Borek Bockal.Uholanzi
ilifanikiwa kupata bao la kusawazisha kipindi cha pili kupitia kwa mlinzi wake
Stefan de Vrij kwa mkwaju wa kickwa.Zikiwa zimesalia dakika
chache mtanange huo ufikie mwisho makosa ya mlinzi wa kulia wa Uholanzi Darly
Janmaat yaliwazawadia bao wenyeji Czech baada ya mpira wa kichwa wa mlinzi huyo
kwa golikipa wake Jasper kugonga mwamba na kukutana na mshambuliaji Vaclav
Pilar aliyeutia kimiani.Mpaka dakika tisini zinatimia Czech 2-1 Uholanzi.
kocha Hiddink |
Baada ya mtanange huo Janmaat alisema
“Hilo ni
kosa langu najisikia vibaya kupoteza mchezo ambao tulipaswa tushinde.Nilikuwa
nikijaribu kumrudishia mpira Jasper kwa bahati mbaya sikuupiga
vizuri.Nilijisikia vibaya sana baada ya tujio hilo”.
GROUP H:
Timu ya taifa ya Italia imeanza vyema harakati za kuhakikisha
kuwa inakuwa moja kati ya timu zitakazofuzu mapema Euro 2016 baada ya kuifunga
timu ngumu ya Norway kwa jumla ya magoli 2-0 katika mtanange uliopigwa huko
Oslo,Norway.
Italia iliyokuwa ikiongozwa kwa mara ya kwanza na kocha mpya
Antonio Conte ilipata magoli yake kupitia mshambuliaji wake Simone Zaza na
mlinzi Leonardo Bonucci.
0 comments:
Post a Comment