Habari na Paul Manjale
Mshambuliaji
wa klabu ya Arsenal anayepambana kuzigusa nyavu za adui japo kwa goli moja tu
Mfaransa Yaya Sanogo ameibuka na kujitetea dhidi ya mashabiki na wadau
mbalimbali wa mpira wanaodai kinda huyo si lilote si chochote klabuni hapo.
Sanogo akishangilia goli dhidi ya Benfica katika michuano ya Emirates |
Sanogo
akiongea na jarida la L ‘Equipe la
nchini Ufaransa amesema “Unapotoka moja kwa moja ligi daraja la pili Ufaransa (ligue
2) na ukakutana na mtu kama vicent
Kompany kwa kweli inakuwa siyo kazi
rahisi. Kwasasa najiona nimepiga hatua.Unajua unapofanya mazoezi na wachezaji
mahiri uwezo wako unaongezeka na unapocheza mechi kubwa unapata uzoefu”
Vicent Kompany mmoja kati ya walinzi wanaomnyima usingizi Yaya Sanogo |
Sanogo
aliongeza “Upokuwa na miaka 21 siyo rahisi sana kucheza nafasi ya ushambuliaji katika klabu
kama Arsenal.Unahitaji kujituma sana ili uweze kuonyesha thamani yako.Mashabiki
wanajua nimefunga magoli mengi sana nikiwa na vikosi vya vijana.
Enzi za Sanogo katika klabu ya Auxerre |
Wanataka nianze
kufunga lakini nawaahidi siku nikifunga goli langu la kwanza kutakuwa hakuna wa
kunizuia tena itakuwa ni magoli na mimi,mimi na magoli”.
Pia
Sanogo amemuonya nyota mpya wa klabu hiyo aliyesajiliwa hivi karibuni Danny
Welbeck kuwa asitegemee kuanza moja kwa moja katika kikosi cha kwanza cha
Arsenal na badala yake ategemee ushindani mkubwa toka kwake.
0 comments:
Post a Comment