Imeandaliwa na Paul Manjale
0717 70 55 48
paul.manjale@yahoo.com
Huenda ukawa na maswali mengi sana juu ya baadhi ya namba
zilizoko migongoni mwa baadhi ya wacheza soka duniani.Wapo wanaopenda kuvaa jezi
zenye namba yoyote ile migongoni mwao lakini wapo ambao bila jezi namba fulani
maisha huwa ni ya tabu na magumu sana kwao.
Hivi umeshawahi kujiuliza kwanini mchezaji fulani anavaa jezi
namba fulani ambayo wewe kwako inaweza kuonekana ni kituko?Ndiyo kwako ni
kituko ila kwake habari ni tofauti kidogo,kuna kitu amekilenga hapo wala
hafanyi hivyo kwa ajili ya kumkera yoyote bali ni kuifurahisha nafsi yake na
maisha yaendelee.
Leo nimeona siyo vibaya nikizungumzia baadhi ya namba na
maana zake ili kujibu maswali lukuki yaliyoko mitaani kwetu kutokana na kila
mtu kuwa na majibu yake ambayo kidogo ni tofauti na ukweli wenyewe.Wafuatao
wanajibu maswali hayo!!
1.
Mario
Balotelli:Je,ni kwanini anapenda kuvaa jezi no 45 katika kila klabu
anayokwenda?
Wakati Mario anakuwa na kuanza kupenyeza
katika kikosi cha vijana cha klabu ya Inter Milan ya Italia aliambiwa achague
kuvaa jezi kati ya no 36-50 akachagua no 45.Hii ni kwasababu 4+5=9 ambayo ni
nafasi anayoicheza uwanjani na kufanikiwa kufunga magoli katika mechi nne
mfululizo akiwa na kikosi cha vijana cha Inter Milan.Hivyo akaamini kuwa hiyo
ni jezi yenye bahati kwake na ndiyo maana kila klabu anayokwenda Balotelli
huanza kuulizia jezi yake no 45 kama ipo.
Ronaldinho
(80),Andriy Shevchenko (76),Mathieu Flamini (84)
Mwaka 2008-09 wakati klabu ya Ac Milan
inawasajili nyota hawa watatu namba zao vipenzi zilikuwa tayari
zimeshachukuliwa na wachezaji waliokuwepo klabuni hapo.Unajua nini
kilifanyika?Hakuna mchezaji/wachezaji waliokubali kuwapa jezi zao nyota hao
wapya hiyo hivyo iliwabidi nyota hao kuchagua jezi kulingana na umri wao wa
kuzaliwa.
Bixente Lizarazu (69)
Mchezaji wa zamani wa timu ta taifa ya
Ufaransa aliichezea klabu ya Bayern Munich akivalia jezi no 69 kwasababu
alizaliwa mwaka 1969 na urefu wake ulikuwa ni 169.
Clint
Dempsey (2)
Mchezaji na nahodha wa timu ya taifa ya Marekani aliichezea klabu
ya Fulham akivalia jezi no 23 lakini alipohamia klabu ya Tottenham Hotspurs alichagua
jezi no 2 kama kielelezo kuwa mbali ya soka pia ana ajira nyingine ya pili
ambayo ni kufanya muziki wa kufoka foka yaani rap na huko anafahamika kwa jina
la Deuce
0 comments:
Post a Comment