Paul Manjale
0717 705548
Aliyekuwa kocha msaidizi wa klabu ya Manchester United Mike
Phelan amesema kitendo cha klabu hiyo kumuuza mshambuliaji Danny Welbeck kwenda klabu ya Arsenal ni kuua utambulisho wa
klabu hiyo kongwe na maarufu zaidi.
Phelan ambaye alikuwa msaidizi namba mbili
wa kocha Alex Ferguson toka mwaka 2008-2013 ameiambia BBC “Welbeck amekuwa
sehemu ya utambulisho wa Manchester United ambao umevunjwa.Nini kitatokea siku
za usoni ,hakuna anayejua lakini tayari utambulisho huo umeshavunjwa.”
Phelan aliongeza “Kila jambo huwa lina mwanzo wake labda huu
ndiyo mwanzo mpya wa kufanya vitu klabuni na labda ndivyo mpira unakoelekea.Je,ni
bora kutazama sasa kuliko mbeleni?alihoji kocha huyo.
Akikikumbuka kizazi cha akina David Beckham,Nick Butt,Paul
Scholes,Garry na Phil Neville kilichobatizwa jina na kuitwa ‘Class of 92’ na
kuja kutawala anga la soka ya England na dunia Phelan anaona ujio wa nyota kama
Angel di Maria,Radamel Falcao,Marcos Rojo,Ander Herrera klabuni hapo ni kuua
shule ya vipaji iliyoko klabuni hapo.
Ni ngumu kwasababu vijana ndiyo huja na kuwa msaada mbeleni
,tunapaswa kuanzia sehemu fulani na kutumaini kuwa zao hilo la vijana litakuja
kuwa ni msaada katika ligi kuu”.
Pia Phelan amesema Welbeck atafanikiwa Arsenal “Yupo katika sehemu ambayo anaweza kucheza
katika sehemu aitakayo na ninadhani hiyo ndiyo sababu iliyofanya achague
kucheza hapo kwa sababu anaamini atacheza nafasi aipendayo,ambayo ni
ushambuliaji.
Klabu kama Arsenal ni klabu nzuri,ni klabu inayoendeshwa
vizuri.Kama unataka kuchagua klabu ya mpira wa miguu basi Arsenal ndiyo jibu
kwa mchezaji”.
.
0 comments:
Post a Comment