KUMBUKUMBU MICHEZONI
Imeandaliwa na Paul Manjale
0717 70 55 48
Jason Mayele huenda siyo jina maarufu sana masikioni na
machoni mwa wapenzi wa soka Tanzania kama ilivyo kwa majina mengine ya
wachezaji toka Congo DRC kama Lomana LuaLua,Tresor Mputu na wengineo wengi.
Mayele akifanya vitu vyake dimbabi dhidi ya Juventus |
Mwili wa Mayele baada ya ajali |
Lakini katika jiji la Chievo nchini Italia na Congo kwenyewe
Jason Nono Mayele ni mmoja katika ya nyota maarufu na wanaoheshimika zaidi kila
inapoitwa leo,siyo tu kwasababu ya kifo chake bali pia kwa mchango wake kwa
klabu yake ya Chievo na timu yake ya taifa ya Congo.
Je,Jason Mayele ni nani?
Jason Nono Mayele kama anavyofahamika zaidi katika mitaa
mingi ya Bussolengo,Italia na Congo alizaliwa tarehe 4 januari 1976 huko
Kinshasa na kufariki tarehe 2 machi 2002 huko Bussolengo Italia.
Kabla ya kifo chake Mayele aliyemudu kucheza vyema nafasi za
ushambuliaji na winga alifanikiwa kuchezea kwa mafanikio vilabu vya Brunoy (1991-1993),LB Chateauroux ya Ufaransa (1993-1999),Cagliari (1999-2001)
na mwisho Chievo (2001-2002).
Kifo chake
Mayele aliyekuwa mmoja kati ya nyota wa Chievo walioweka
rekodi ya kuipeleka klabu hiyo katika michuano ya Ulaya katika msimu wake wa
kwanza tu katika ligi ya Seria A alifariki akiwa na miaka 26 katika ajari mbaya
ya gari.
Gari alilokuwemo Jason Mayele likiwa limeharibika vibaya |
Mayele aliyekuwa akiliwahi basi la klabu yake la Chievo kwa
ajili ya kwenda kwenye mchezo wa ugenini wa ligi ya Seria A dhidi ya klabu ya Parma, gari
dogo alilokuwa akilitumia liligongana uso kwa uso na gari jingine na kukatisha
uhai wa nyota huyo kutokana na majeraha makubwa aliyoyapata katika sehemu
mbalimbali za mwili wake wakati akiwahishwa hospitali ya karibu katika mji wa Verona.
Jezi yake yastaafishwa
Uongozi wa klabu ya Chievo uliamua kuistaafisha jezi no 30
iliyokuwa ikivaliwa na Jason Mayele ili kutoa heshima kwa nyota huyo aliyekufa
katika mapambano ya kuitetea klabu hiyo.
Rest in peace my old brother jason
ReplyDelete