MAKALA YA LEO
Na Mkubwa Kambi
Liverpool
msinipotezee mwanangu!!
Ninaipenda kweli Liverpool lakini mwanangu nampenda zaidi, hii ni
kinyume na mwanangu mwenyewe, yeye anaonekana kuipenda zaidi Liverpool
kuliko anavyonipenda mimi (ni utoto tu akikua ataacha), ukiona siku
amenibeep basi anaomba kibali akaitazame Liverpool kwenye Luninga.
Liverpool bado haijakaa vyema, na hakuna mpaka sasa anayejua tatizo la
Liverpool liko wapi? mbaya zaidi hata Brendan Rodgers pia hajui tatizo
la timu yake!!, bench la ufundi la Liverpool hawajui tatizo la timu
yao!!, mashabiki damu wa Liverpool hawajui tatizo la timu yao!!
Ingia kwenye mitandao yoote ya Liverpool hivi sasa wanagombana tu
wenyewe kwa wenyewe, wale wenye mioyo ya chura (mioyo isiyo na
uvumilivu) ndio kabisa kila kukicha ni kulaumu.
Bahati mbaya zaidi Liverpool hata hapa Tanzania ina washabiki wenye
kuheshimika sana (amini maneno yangu) washabiki ambao hawana kelele,
mashabiki ambao ni Die Hard,Hata Mr. Liverpool Ezekiel Kamwaga naye
simuoni tena akiandika kwa mbwembwe kuhusu Liver yeke!! hata wachambuzi
wetu wa magazeti kwa kuwa nao ni wanajamii wanaogopa kuandika ukweli
kuhusu Liverpool nadhani wanatuonea haya! Si marafiki zatu na
wanatuheshimu, lakini lingine wanajua kuwa Liverpool haitabiriki inaweza
kuamka wakati wowote! Unabisha? kwani ulijua kama mwaka jana wangeweza
kuwa juu ya timu yako iliyosheheni wachezaji World Class, timu yako
yenye mashabiki wenye kelele kila kona?!!
Baada ya kuitazama Liverpool kwa jicho huru, baada ya kuamua kuweka
pembeni mahaba niue nimepata mwanga kidogo wa kugundua matatizo ya
Liverpool.
1. Nafasi waliyoishika msimu uliopita;- Kama nilivyotangulia kusema
awali nafasi waliyoikamata Liverpool mwaka jana ilikuja kama surprise
japo ilisababishwa na jitihada za pamoja kama timu kuanzia wachezaji,
benchi la ufundi na support ya Empire Of The Kop L.F.C ambayo huwa
haipotei, kwa kushika nafasi ya pili kwenye ligi na kuwa mpigania
ubingwa hadi mechi ya mwisho kila mmoja ndani ya Liverpool nafasi pekee
iliyopo kwenye fikra zao ni ubingwa ikishindikana kubaki Top 4 na ili
jambo hilo liwezekane hii timu ilihitajika ianze ligi ikiwa ile ile
iliyomaliza ligi bila kumpoteza mchezaji hata mmoja, kama ni wachezaji
wapya walipaswa kuingia pole pole kwa kumbadilisha mchezaji mmoja mmoja
kwa awamu.
2. Kutokuwa na First Eleven:- Liverpool hadi sasa baada ya kucheza mechi
nne za EPl na moja ya ligi ya mabingwa bado haina First Eleven,
wachezaji wenye uhakika wa namba ni watano tu pamoja na Nahodha
aliyechoka, (Simon Mignolet, Martin Skirtel, Alberto Moreno, Steering,
na Daniel Sturridge) wengine wote hujui nani ataanza leo nani ataingia
sub hili ni tatizo kubwa pia kwani inaonekana limewaingia hata wachezaji
wenyewe hivyo kukosa maandalizi ya kiakili ya mchezo unaofuata,
mchezaji anapojua atakuwemo kwenye kikosi cha juma lijalo humfanya
aisumbue akili yake kuwa kitu gani bora atakifanya kwa faida yake na
faida ya timu kiujumla.
3) Kikosi kujaa wachezaji Standard:- Liverpool ilimaliza msimu uliopita
ikiwa na wachezaji World Class wawili tu, Steven George Gerrard na Luis
Suarez ambacho ilipaswa kupigania ni kuongeza watu wa kaliba hiyo japo
wawili bahati mbaya kwao ikawalazimu kumuuza LUIS SUAREZ ambaye ndiye
alikuwa roho ya timu na wakaingiza wachezaji karibu wanane ambao ni
wachezaji wa kawaida (Ukiondoa Balloteli pekee), hii imeigharimu sana
timu, unapokuwa na wachezaji wa aina hii inakuwa ni ngumu kupata matokeo
kwenye mchezo ambao timu pinzani imewazidi mbinu za kimchezo, faida ya
kuwa na wachezaji ambao ni World Class ni pale timu inapozidiwa mbinu za
kimchezo ndipo vipaji binafsi pamoja na uzoefu vinapofanya kazi ya
kuamua matokeo Liverpool ya sasa inamtegemea Steering pekee ndio afanye
kazi hii pia faida nyingine wachezaji hawa huingia moja kwa moja katika
kikosi cha kwanza unless otherwise wakute wachezaji wa kaliba yao
kikosini, .
4) Kukosekana mhimili wa timu (beki):- Nyumba imara zote duniani huanza
kujengwa msingi ulio imara na kwenye timu za soka timu ii iwe imara
huitaji kuwa na beki imara, msimu uliopita Liverpool haikuwa na beki
imara! ilipata bahati ya kuwa na kiongozi imara kwenye safu ya ulinzi
Martin Skirtel aliyekuwa na wasaidizi wawili pembeni yake Agger na
Mamadou Sakho ambao walijenga safu nzuri sana pongezi kwake kijana
Flanagan ambaye alikuja kuisakafia vyema hii ngome, msimu huu kuna
maingizo matatu mapya kule nyuma, Manquillo, Moreno na Lovren katika
hali ya kawaida wanahitaji kupewa muda ili wajenge ukuta ulioimara, je
ligi inawasubiri wao? jibu unalo wewe shabiki wa Liverpool, Bahati mbaya
zaidi timu imekosa kiungo mkabaji, kiungo mkabaji pekee aliyepo pale
Liverpool ni Lucas Leiva bahati mbaya BR amepoteza uaminifu kwake.
5) Majeruhi:- Hii nayo wakati mwingine ni mipango ya Mungu yeye anapanga
sisi tunapangua, Flanagan, Sturridge, Coutinho, hata Skirtel wameingia
kwenye group la wagonjwa, wachezaji hawa walimaliza ligi ya msimu
uliopita wakiwa kwenye kikosi cha kwanza, timu inapokosa wachezaji wanne
waliomaliza vyema msimu uliopita huku ikiwa na maingizo mapya karibu
sita ni pigo kubwa, kwenye hili tuzidi kumba Mungu wachezaji wote wawe
fit ili kumpa mwalimu chaguo sahihi.
Nini kifanyike?
1) Katika sheria za soka wachezaji wa ndani wakifika saba timu
inaruhusiwa kucheza mechi na hawa ndio wachezaji pekee wa Liverpool
ambao Brendan Rodgers hapaswi kuwaweka bench kuwaweka bench labda wawe
majeruhi (Moreno, Skirtel, Jordan Henderson, Steering, Coutinho,
Sturridge na Balotelli) hapa ndipo msingi wa kujenga First eleven
uanzie.
2) Hili washabiki wengi wa Liverpool hawataki kulisikia, ndugu zangu,
nguvu kitu cha kwisha, tulikuwa na kina Mohammed Ally,Mike Tyson, n.k
leo hii wako wapi kama ingekuwa ni draft ama bao hadi hii leo
tungeendelea kuwa nao. Steven Gerrald anapaswa kuchaguliwa baadhi ya
mechi, hasa kwa ile position anayoitumikia sasa hivi ni kumtafutia
malipo ya uzeeni yasiyostahili, Brendan Rodgers weka Lucas pale, bahati
mbaya msimu uliopita alikabiliwa na majeruhi mkabidgi majukumu pale ama
la train Jordan Henderson aanze kuitumikia nafasi ile kwa style yake ya
uchezaji ndani ya mechi nne tu atakuwa ameshayajua majukumu yake.
3) Liverpool itengeneze mfumo wa kushambulia kupitia kwa Mario
Balotelli, wachezaji wote wacheze kumzunguka yeye ni mtu mwenye miguu
yenye macho, misuli yenye nguvu, mwepesi kupinduka anapoliona goli
mwisho ni mshindani halisi, bahati mbaya sana hadi sasa mashuti karibu
yote aliyopiga Balotelli kuelekea golini pamoja na magoli aliyofunga ni
juhudi zake binafsi. Timu yoyote duniani ingemhitaji Balotelli ukiondoa
kasoro zake ambazo ni Mungu pekee anayeweza kumuepusha nazo.
Mwisho kabisa ule mpango wa kumnyakua Víctor Valdés ufanywe haraka ili
Mignolet apate mshindani halisi, apate changamoto ya kutosha.
Zaidi ya yote You will never walk alone.
0 comments:
Post a Comment