Mshambuliaji hatari wa klabu ya Everton Romelu Lukaku
amesema klabu ya Liverpool ni kama vilabu vingine tu hivyo kufungika
inawezekana.Lukaku ameyasema hayo kabla ya kuikabiri klabu hiyo katika mchezo
wa watani wa jadi utakaopigwa katika dimba la Anfield leo jumamosi.
Liverpool inaingia katika mchezo huo ikiwa imecheza jumla ya
michezo mitano na kufungwa mitatu huku ikiwa imefanikiwa kushinda miwili pekee
haionyeshi kumtia hofu yoyote Lukakau.
Amesema “Kila mtu anaongea kuhusu Everton hakuna anayeongea
kuhusu Liverpool.Wanafungika,siko hapa kukosoa.
“Nawaheshimu Liverpool kama wao wanavyopaswa kutuheshimu
sisi.Tuna kikosi kizuri ambacho naamini tukianza kushinda itakuwa vigumu
kutuzuia.Mchezo huu ni muhimu kwetu kwani tunaweza kuanzia hapa kuandika
historia mpya.Tumekuja Anfield mara sita,tumepoteza mara nne na kupata sare
mara mbili nadhani huu ni wakati wetu kushinda”
0 comments:
Post a Comment