Mlinzi mpya wa klabu ya
Bayern Munich Mmorocco Mehdi Benatia (27) ambaye hivi karibuni ametua klabuni hapo
kwa kitita cha euro 27 akitokea klabu ya As Roma ya Italia amesema bila ya
mchezo wa soka hajui leo hii angekuwa wapi.
Benatia ambaye ni zao
la baba Mmorocco na mama Mualgeria alikulia pembezoni mwa jiji la Paris (Ufaransa)
ambako takwimu za uharifu kwa mujibu wake ziko juu mno,anasema soka ndiyo ilikuwa njia pekee ya kumuweka mbali na
matatizo hayo.
Akifanya mahojiano na jarida
la Kicker la nchini Ujerumani Benatia amesema
“Nisingeweza
kuwa daktari au injiania,wazazi wangu hawakuwa na fedha za kutosha hivyo
hakukuwa na jinsi ilibidi nitafute njia.Soka imeniokoa,sijui hali ingekuwaje
nisingekuwa katika upande huu wa maisha”.
Benatia aliibuliwa na
wasaka vipaji vya soka maarufu kama scouts akiwa na umri wa miaka 13 na kupelekwa katika
shule zilizoko jijini humo ili kuendeleza kipaji chake .Akikumbuka tukio hilo
Benatia anasema
“Niliondoka
eneo lile na hilo lilikuwa ni jambo zuri kwangu.Soka ilikuwa ni muhimu mno.Kwa
watoto wote pale soka ilikuwa ni njia ya kuachana na kila kilichoendelea
pale.Sikufanya vizuri darasani,sikuwa msikivu ilikuwa ni eneo gumu sana kuishi
nashukuru soka imeniokoa.
0 comments:
Post a Comment