Kiungo wa
kimataifa wa England Jack Wilshere amefurahishwa na kiwango alichokionyesha
usiku wa jana katika mchezo wa kusaka tiketi ya kufuzu michuano ijayo ya Ulaya
dhidi ya timu ya taifa ya Uswisi uliopigwa katika dimba la Jacob Park mjini
Basel.
Wilshere
ambaye alicheza nafasi ya kiungo wa ulinzi ameelezea furaha yake kwa kusema
“ Nawapongeza
wachezaji wenzangu kwa ushindi mkubwa wa bao 2-0 tulioupata dhidi ya wenyeji
Uswisi kwakweli ulikuwa ni mchezo mgumu mno, wapinzani wetu walicheza kwa nguvu
na maarifa makubwa sana”.
Pia nina
furaha kwa kucheza vizuri katika nafasi mpya niliyoagizwa kucheza na kocha Roy
Hodgson kama kiungo wa ulinzi.Sikuwahi kuicheza nafasi hii kabla.Niliongea na
kocha pamoja na Garry Neville kabla ya mchezo wakaniambia wanataka nicheze
nafasi hiyo na nimeifurahia kwakweli”.
“Ilikuwa
ni mara yangu ya kwanza kucheza nafasi hiyo nadhani baada ya mazoezi makali na
kutazama video ya mchezo huo pamoja na za viungo mahiri kama Pirlo na
Mascherano nitaimarika sana”
0 comments:
Post a Comment