Klabu ya Liverpool inapanga kuanza haraka mazungumzo ya
kumuongezea na kumboreshea mkataba nyota wake Raheem Sterling ambaye ameanza kuwindwa na klabu ya Real
Madrid ya Hispania.
Kutoka kambi ya klabu hiyo ya Merseyside habari zinasema
Sterling (19) ambaye bado ana mkataba na Liverpool mpaka mwaka 2017 huku
akipokea mshahara wa paundi
30,000 kwa juma ameandaliwa maboresho makubwa yatakayomfanya avune zaidi ya paundi 100,000 ili aendelee kukipiga Anfield kwa miaka mingine mingi.
30,000 kwa juma ameandaliwa maboresho makubwa yatakayomfanya avune zaidi ya paundi 100,000 ili aendelee kukipiga Anfield kwa miaka mingine mingi.
Sterling ni kati ya nyota bora na tegemeo katika kikosi cha
Brendan Rodgers msimu huu hasa baada ya kuondoka kwa mshambuliaji Louis Suarez
aliyetimkia klabu ya Barcelona ili kumfanya atulize akili yake klabuni hapo
mkataba mnono uko mezani kwa ajili yake.
0 comments:
Post a Comment