Klabu ya Arsenal huenda ikazikosa
huduma za mlinzi wake wa kulia Mfaransa Mathieu Debuchy kwa muda wa miezi
miwili au zaidi kufuatia maumivu ya kifundo cha mguu aliyoyapata katika mchezo
wa ligi kuu dhidi ya Manchester City uliopigwa katika dimba la Emirates.
Debuchy alitolewa nje kwa machela
dakika ya 81 ya mchezo kufuatia kujikwaa na kuangua wakati akijaribu kumiliki
mpira kulikopelekea kuumia kwa kifundo cha mguu wake wa kushoto.Vipimo vya
awali vimeonyesha kuwa mlinzi huyo hajavunjika kama ilivyodhaniwa na badala
yake vinasubiriwa vipimo vingine (scanning) ili kubaini ukubwa wa jeraha na
muda wa matibabu ambao unahisiwa utakuwa kati ya miezi miwili mpaka mitatu.
Kufuatia kuumia kwa
Debuchy,Arsenal inabaki na walinzi watano wanaopaswa kuziba nafasi tano
zilizoko katika idara hiyo huku kinda Calum Chambers akichukua jukumu la
kucheza nafai ya ulinzi wa kulia katika mchezo wa jumanne wa ligi ya mabingwa
dhidi ya Borussia Dortmund.
Debuchy mbali ya kuukosa mchezo
dhidi ya Dortmund pia atakozikosa mechi kadhaa za ligi zikiwemo dhidi ya Spurs
na Chelsea pamoja na Galatasaray na Anderletch kwenye ligi ya mabingwa.
Akizungumzia hilo kocha Wenger
alisema “Hakuna mvunjiko wowote
alioupata lakini ni jeraha kubwa.Ni baya na siyo zuri hata kidogo
0 comments:
Post a Comment