Mlinda mlango wa klabu ya Real
Madrid Iker Casillas amekubali baadhi ya
lawana zinazoelekezwa kwake toka kwa mashabiki wa klabu hiyo baada ya kipigo
cha goli 2-1 toka kwa wapinzani wao wa mji mmoja Atletico Madrid katika mchezo
wa La Liga uliopigwa juzi jumamosi katika dimba la Santiago Bernabeau.
Casillas,33,ambaye siku hiyo alikuwa
akicherekea kufikisha miaka 15 tangu aanze kuidakia timu hiyo alijikuta akianza
kuyapata machungu ya mashabiki wa klabu hiyo baada ya wageni Atletico Madrid kutangulia
kupata bao dakika ya 10 ya mchezo kwa kichwa cha karibu cha kiungo Tiago Mendez.Baada
ya bao hilo mashabiki hao walianza kumzomea mlinda mlango huyo wakidai alipaswa
kufanya kitu cha ziada badala ya kuruhusu bao ambalo wao wanaliona ni la
kizembe.
Casillas ambaye ameichezea klabu
hiyo michezo 684 akifanya mahojiano na Canal Plus Tv alisema
“Mashabiki ndiyo wenye kauli ya mwisho na wakifikiri wanapaswa wakuzomee huna budi kukubali na kuheshimu
mawazo yao.Ni haki yao na ninachopaswa kufanya ni kuwajibu kwa njia/namna
niijuayo,kwa kucheza mpira”.
Akihojiwa kuhusu kuendelea
kufungwa mipira ya kutenga (set pieces) Casillas alisema “Nalijua tatizo hilo ambalo kwa kiasi kikubwa linatokana na kupoteza
kujiamini kunakopolekea tuendelee
kuruhusu magoli mengi ya set pieces,mimi kama mlinda mlango nawajibika kwa
hilo.
“Nawajibika kwa hilo na ninapaswa kukubali baadhi ya lawama hizo.Kati
yetu tunapaswa kulitatua tatizo hilo ambalo linakuwa siku hadi siku”.Alimaliza
Casillas ambaye ameshaisaidia klabu hiyo kushinda mataji matatu ya ligi ya
mabingwa,mataji mawili ya Copa del Rey na matano ya La Liga.
0 comments:
Post a Comment