Kama unadhani ujio wa kocha Mdachi Lous Van Gaal katika klabu ya
Manchester United ni wa mchezo mchezo tu basi sikia hii.
Kocha huyo ambaye kiuhalisia ni mkali na asiyependa masihara hata
kidogo amuibuka na mpya mapema wiki hii baada ya kuwanyoonyesha kidole cha
shahada nyota wake wanaoongea Kihispania wakiongozwa na winga Antonio Valencia na
kuwataka wajifunze lugha ya kiingereza haraka vinginevyo hali itakuwa mbaya
kwao.
Van gaal amefikia hatua hiyo ili kurahisisha mawasiliano kati yake na
wachezaji wake ama wachezaji kwa wachezaji wakati wote wa mazoezi na mechi.Tayari
kocha huyo ameshawaanzishia darasa maalumu nyota wake wageni ili kuhakikisha
wanaimudu lugha hiyo adimu.Nyota ambao tayari wameshaanza makamuzi (kujifunza)
ni Marcos Rojo na Angel di Maria ambao wameanza hatua ya awali kabisa yaani “beginners
“hawa wanapata tuisheni mara mbili kwa wiki.Falcao,Herrera na David de Gea hawa
kidogo wanajitahidi wameweka katua ya kati yaani “Intermediate”.
Inasemekana Antonio Valencia ambaye mpaka sasa ameshaishi England kwa
miaka minane tangu atue nchini humo mwaka 2006 akiwa na miaka 20 tu hajawahi
kufanya mahojiano (interview) kwa lugha ya kiingereza.Hii inatokana na tabia ya
aibu aliyonayo nyota huyo mzaliwa wa Ecuador hata kufikia kumuomba Van gaal
ampatie darasa la peke yake bila kuchanganyika na wenzake.
Hatua hii ya Van gaal imepokelewa kwa mikono miwili na mashabiki wa
klabu hiyo ambapo hapo awali walianza kuwa na mashaka na kule United ilikokuwa
ikielekea na kuhisi kupotea kwa utambulisho wa klabu hiyo hasa baada ya kuleta
nyota wengi wakubwa huku wazawa kama Danny Welbeck na Tom Cleverly wakionyeshwa
mlango wa kutokea.
0 comments:
Post a Comment