Paul Manjale
0717705548
Ikiwa leo ndiyo mwisho wa usajili barani ulaya pata kujua
machache yatakayojili ndani ya saa kadhaa zijazo….
STAMFORD BLIDGE: Klabu
ya Chelsea imemtoa kwa mkopo kiungo wakeMdachi Marco Van Ginkel (21) kwenda klabu ya Ac Milan ya Italia wakati
huo huo kiungo mwingine wa klabu hiyo Mscottland Islam Ferouz amerejea klabuni
hapo zikiwa ni saa 48 tu tangu atue kwa
mkopo katika klabu ya Kylia Soveton Samara inayoshiriki ligi daraja la pili
nchini Urusi kwa madai kuwa bado hakuwa tayari kuanza maisha mapya hapo baada
ya awali kupata tabu kuzoea England.
EMIRATES:Kutoka
gazeti kubwa na maarufu la michezo nchini Ureno O jogo habari zinasema kinda wa
klabu ya Arsenal Joel Campbell ameomba kutimka klabuni hapo na kujiunga na klabu
ya Benfica.O jogo linasema Campbell ameomba kuondoka baada ya kuhisi huenda
kocha Arsene Wenger bado hayuko tayari kumtumia katika kipindi hiki.Hivi
karibuni klabu ya Benfica ilifanya mawasiliano na klabu ya Arsenal kutaka
kumsajili nyota huyo kwa uhamisho wa mkopo ama wa kudumu na kuwa tayari kulipa
kitita cha Euro milioni 10.
ETIHAD:Mshambuliaji
Alvaro Negredo amekubali kutua Valencia kwa mkataba wa mkopo wa msimu mmoja
wenye kipengere cha uhamisho wa kudumu ili kumpisha mshambuliaji Radamel Falcao
anayewaniwa kwa udi na uvumba na klabu ya Manchester City
0 comments:
Post a Comment