Imetayarishwa na Paul Manjale
0717 705548
RADAMEL FALCAO GARCIA ZARATE
Wakati dirisha la usajili likifungwa usiku wa septemba mosi
gumzo kubwa England na duniani kote lilikuwa ni usajili wa mshambuliaji hatari
raia wa Colombia Radamel Falcao Garcia Zarate
(El Tigre/mfalme wa ligi ndogo ya Ulaya maarufu kama Europa League)
kutua klabu ya Manchester United kwa uhamisho wa mkopo wa msimu mmoja.
Falcao ambaye alizaliwa tarehe 10 Februari 1986 huko Santa
Marta,Colombia ni mtoto wa mchezaji wa wa zamani wa nafasi ya ulinzi wa timu ya taifa ya nchi hiyo Radamel Garcia.Falcao
ametua Manchester United kwa ada ya
mkopo ya paundi milioni 6 huku kukiwa na kipengere cha kumsajili moja kwa moja
mwishoni mwa msimu kwa kitita cha paundi milioni 43.5.
Je,jina Falcao lilitoka wapi?
Radamel alipewa jina
Falcao na baba yake mzazi kutokana na mzazi huyo kuwa na mapenzi makubwa na
nyota wa zamani wa nafasi ya kiungo wa timu ya taifa ya Brazil na klabu ya As
Roma Paulo Roberto Falcao.Paul Roberto Falcao aliyetamba sana miaka ya 80s na
kuwa mchezaji ghali zaidi kipindi Fulani inasadikika kuwa ni mmoja kati ya viungo
bora zaidi timu ya taifa ya Brazil kuwahi kuwa nao.
Je,baadhi ya makocha wanamzungumziaje?
Fabio Capello “Radamel
Falcao yuko daraja moja na nyota kama Lionel Messi na Christiano Ronaldo”……….
Pep Guadiola “Falcao
ni mchezaji wa ajabu,na ni mmoja kati ya wachezaji wenye vipaji vikubwa sana
vya soka duniani”
Afunga goli 5 peke yake katika mchezo mmoja wa La Liga.Ilikuwa
ni desemba 9,2012 katika mchezo wa ligi uliopigwa katika dimba la Vicente
Cardeloni ambapo Atletico Madrid walishinda jumla ya bao 6-0 huku Falcao
akiweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga goli 5 ndani ya muongo mmoja katika
mchezo mmoja wa ligi ya La Liga.
Je,kipi kingine kilimvutia baada ya Monaco kumtaka?
Mbali ya mshahara mzuri na mambo mengine binafsi Falcao alisema “Nimetua Monaco kufuata nyayo za Thierry Henry ambaye alipita hapa na
kuwa nyota mkubwa duniani.Nampenda sana Henry nimekuwa shabiki wake mkubwa
hivyo uwepo wangu hapa ni kuenzi japo kidogo kile alichofanya na alikopitia”
Je,goli lake la kwanza akiwa na timu ya taifa alilifunga
akiwa na umri gani?
Ilikuwa ni katika mchezo wa kombe la Kirin Cup uliopigwa
huko Japan.Falcao alifunga goli pekee na la ushindi katika mchezo huo dhidi ya
Montenegro.
Je,alianza soka la ushindani akiwa na miaka mingapi?
Falcao alinza kucheza soka katika timu ya daraja la pili
nchini Colombia maarufu kama Categoria Primera B tarehe 28 Agasti 1999 akiwa na
umri wa miaka 13 na siku 199 na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji mdogo zaidi kuwa
kucheza ligi ya kulipwa ya nchi hiyo.
Februari 2001 Falcao alitua Argentina kuichezea klabu ya
River Plate kwa dau la dola 500,000 na kuanza kukichezea kikosi cha vijana cha
klabu hiyo kilichokuwa ligi daraja la nane kabla ya kupandishwa kikosi cha
kwanza mwaka 2005 na kocha Leonardo Estrada.
0 comments:
Post a Comment