Habari na Paul Manjale
Nyota wa zamani wa Brazil Pele
amewataka wachezaji wanaocheza ligi ya
nchi hiyo kufuata mfano wa mlinzi wa kulia wa Barcelona Dani Alves katika
mapambano yao dhidi ya ubaguzi wa rangi michezoni na kuacha kulikuza tatizo
hilo kwenye vyombo vya habari .Hii imekuja kufuatia kufungiwa kwa klabu ya
Gremio kutokana na vitendo vichafu vya ubaguzi
toka kwa mashabiki wake dhidi ya mlinda mlango mweusi wa Santos.
Pele ameyazungumza hayo hivi
karibuni kufuatia kikundi cha mashabiki
wa klabu ya Gremio ambao ni mabingwa mara nne wa taji la ligi maarufu kama
Brazilian Cup (Copa Dos Brasil) ambalo ni taji la pili kwa ukubwa nchini kumfanyia vitendo vya kibaguzi pamoja na
kumuita nyani mlinda mlango wa klabu ya Santos,Mário Lúcio Costa Duarte,Aranha
katika mchezo uliopigwa katika dimba la Arena Gremio huko Porto Alegre na Santos kuibuka na ushindi
wa goli 2-0.
Aranha akilalamika kwa mwamuzi baada ya kubaguliwa na mashabiki wa Gremio |
Kufuatia kosa hilo mahakama ya
michezo imeamua kuitoa mashindanoni klabu hiyo inayofundishwa na kocha Felipe
Scolari pamoja na kuipiga faini ya dola 20,000 huku mwanamke wenye umri wa miaka 23 aliyetambuliwa kuwa
ndiye chanzo cha kadhia hiyo akifungiwa kujihusisha na masuala yote ya soka kwa
miaka miwili.
Aranha akiwa mazoezini |
Pele amesema “Mwaka jana,wakati Alves anaenda kupiga kona,kuna mtu alimtupia ndizi
uwanjani.Aliimenya ndizi ile,kuila na akapiga kona ile.Hakuna aliyeongelea tena
swala lile.Kilikuwa na kitendo cha ubaguzi.Nadhani kama Dani angeichukua ile
ndizi na kuitupa,tungekuwa tunaliongelea tukio hilo mpaka leo.
Mashabiki wa Gremio |
“Nafikiri Aranha alijivuruga kidogo baada ya kutaka kugombana na
mashabiki wa Gremio.Kama ingekuwa ni kususa ama kulalamika kwa mwamuzi kila
mara tangu nilipoanza kucheza soka hapa Brazil,Latin America na kwingineko,kila
nilipokuwa nikifanyiwa vitendo vya kibaguzi basi kila mchezo ungekuwa
unasimamishwa”.
“Kuna wakati Santos ilikuwa na Dorval, ambaye alikuwa ni mweusi akicheza winga,Pele alikuwa mweusi.Mengalivio alikuwa mweusi
pamoja na Coutinho.Santos tulikuwa mabingwa wa dunia huku Pepe akiwa
mzungu pekee katika kikosi kizima.Tulipokuwa tukicheza katika maeneo ya ndani
ndani ya Brazil (vijijini) tulikuwa tukiitwa majina ya ajabu ajabu.Je,mliwahi
kusikia habari zozote za ubaguzi wakati huo?Ni kwa sababu tulikuwa hatulitilii
mkazo suala hilo.Unapoliongea sana jambo ndivyo unavyozidi kulikaribisha”.Alimaliza
Pele
0 comments:
Post a Comment