Ama kweli dunia ina mambo!!kama huamini sikia hii.Mlinzi wa zamani wa
klabu ya Manchester United Rio Ferdinand amesema moja kati ya sababu kubwa za
kikosi cha United kuvurunda msimu uliopita ni kutokana na aliyekuwa kocha wao
wakati ule David Moyes kuwapiga marufuku kula chips jioni kabla ya mechi.Upo?
Hii ni moja katika ya tuhuma kibao dhidi ya David Moyes zilizoko katika
kitabu cha Ferdinand kiitwacho 2sides ambacho
kimeanzwa kuchapishwa kwenye gazeti la The Sun la
Uingereza.
Rio amesema “Ilikuwa ni desturi yetu kula Chips jioni kabla ya mechi lakini Moyes
alipoingia aliuvunja utaratibu huo na hapo ndipo balaa lilipoanza.Jiulize nini
kilitokea muda mfupi baada ya Moyes kutimuliwa na Ryan Giggs kuchukua timu?
“Dakika ishirini baada ya Moyes kuondoka tulikuwa juu ya baiskeli zetu
tukipasha misuli moto na mwenzetu mmoja akasema {Mnajua nini?Tumvae
Giggs.Tunapaswa kumvaa na kumwambia aturudishie chips zetu.
Pia katika kitabu hicho Ferdinand amemsifia Alex Ferguson kuwa ni kocha
bora zaidi kuwahi kumfundisha.Amesema “Ferguson alikuwa ni
kocha muungwana mno hata kuwaomba
msamaha wachezaji wake pindi alipowakosea.Ni kocha anayejua kupata kile
anachokihitaji toka kwa mchezaji wake”.Tofauti na Moyes ambaye alileta mbinu za timu ndogo kwenye timu kubwa.
0 comments:
Post a Comment