Addis Ababa,Ethiopia.
Kenya imeifunga Uganda Cranes kwa mabao 2-0 katika mchezo wa kundi B wa michuano ya Cecafa Chalenji Cup uliopigwa jioni ya leo huko Addis Ababa, Ethiopia.
Kenya ambao ni mabingwa watetezi wa michuano hiyo wamepata magoli yao kupitia kwa Jacob Keli aliyefunga dakika ya 29 akiunganisha krosi safi ya Eric Johanna.
Goli la pili la Kenya limefungwa dakika ya 49 na Micheal Olunga aliyeingia kuchukua nafasi ya Jacob Keli aliyeumia.
Kufuatia ushindi huo Kenya imefanikiwa kuongoza kundi B ikiishusha Burundi ambayo jana iliifunga Zanzibar kwa goli 1-0.
Michuano hiyo itaendelea tena kesho kwa michezo ya kundi C kupigwa huko Bahir Dar ambapo Sudan Kusini watavaana na Djibouti huku wageni Malawi wakivaana na Sudan.
0 comments:
Post a Comment