728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, November 29, 2015

    ETOILE DU SAHEL YATWAA UBINGWA WA SHIRIKISHO AFRIKA,YAITUNGUA ORLANDO PIRATES

    Klabu ya soka ya Etoile du Sahel kutoka Tunisia ndio mabingwa wa taji la Shirikisho barani Afrika mwaka 2015.

    Sahel walikabidhiwa taji hilo baada ya kuishinda Orlando Pirates ya Afrika Kusini kwa
    jumla ya mabao 2 kwa 1.

    Fainali ya pili ilichezwa Jumapili jioni mwishoni mwa juma jijini Tunis na mabingwa
    hao kupata bao la mapema katika dakika ya 24 kipindi cha kwanza.

    Ahmed Jebal ndiye alifunga bao hilo baada ya mabeki wa Orlando Pirates kujichanganya kutokana na mashambulizi kutoka kwa
    wapinzani wao.

    Juhudi za Orlando Pirates kusawazisha bao walilofungwa ziliambulia patupu baada ya kulemewa katika safu ya kati.Fainali ya kwanza wiki moja iliyopita, timu zote mbili zote sare ya bao 1 kwa 1 jijini Johannersburg.

    Hili ni taji la pili kwa Etoile du Sahel kushinda baada ya lile la mwaka 2006 lakini mwaka
    2008 ilimaliza ya pili walipokutana na watani
    wao CS Sfaxien pia kutoka Tunisia.

    Hakuna klabu ya Afrika Kusini ambayo imewahi kushinda taji hili la Shirikisho katika
    historia ya mashindano haya.

    Etoile du Sahel pamoja na kutuzwa kombe hilo wamejishindia pia Dola za Marekani 625 na itachuana na TP Mazembe ya DRC bingwa wa taji la klabu bingwa barani Afrika kuwania
    taji la Super Cup mwezi Februari mwakani.




    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ETOILE DU SAHEL YATWAA UBINGWA WA SHIRIKISHO AFRIKA,YAITUNGUA ORLANDO PIRATES Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top