728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, November 19, 2015

    HAKUNA KUAMINIANA TENA:KIUNGO UBELGIJI AITIWA POLISI AKIDHANIWA GAIDI


    Antwerp,Ubelgiji.

    Jumanne ya wiki hii nusura iwe mbaya kwa kiungo wa Ubelgiji na AS Roma Radja Nainggolan baada ya kuitiwa polisi akidhani kuwa ni gaidi.

    Kiungo huyo 27 alikutwa na tukio hilo katika hoteli ya Radisson, Antwerp alipokuwa akila bata baada ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati ya Ubelgiji na Hispania kuahirishwa kwa hofu ya ugaidi.

    Wageni waliokuwa wamepanga katika hoteli hiyo maarufu mjini Antwerp walipata hofu baada ya kumuona mtu mmoja mwanaume amenyoa kiduku huku mwili wake ukiwa umejaa tattoo na hapo ndipo walipoamua kuwaita polisi ili kuja kumtia nguvuni.

    Lakini baada ya polisi kufika hotelini hapo waliishia kucheka tu na kuwaambia watu waliowaita kuwa mtu wanayedhani ni gaidi ni kiungo wa timu yao ya taifa ya Ubelgiji anaitwa Radja Nainggolan.Ikabidi wapige nae picha.

    Asili yake 

    Radja Nainggolan amezaliwa na baba Mbelgiji huku mama akiwa Muindonesia.

    Je,anasemaje baada ya tukio hilo?

    Radja Nainggolan amekiri kuwa una muonekano unaotisha lakini ameshukuru polisi kumtambua vinginevyo ingekuwa balaa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HAKUNA KUAMINIANA TENA:KIUNGO UBELGIJI AITIWA POLISI AKIDHANIWA GAIDI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top