728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, November 15, 2015

    BIFU KALI:ROBBEN KUTUA MAN UNITED MWEZI JANUARI KISA LEWANDOWSKI

    Munich,Ujerumani.

    Klabu ya Manchester United imeripotiwa kufikiria kumsajili winga wa klabu ya Bayern Munich Arjen Robben hapo mwezi januari mwakani ili kuongeza kasi katika safu yake ya ushambuliaji ambayo imepoteza makali yake siku za hivi karibuni.

    Kitu kingine kinachoipa Manchester United nguvu ya kumfukuzia Robben ni bifu kali lililopo kati ya winga huyo na mshambuliaji Robert Lewandowski ambalo siku za hivi karibuni limeonekana kushika kasi.

    Chanzo cha bifu hilo inadaiwa kuwa Lewandowski amemwambia kocha Pep Guardiola kuwa anataka kucheza pamoja na Kingsley Coman au Douglas Costa badala ya Robben ambaye ni mbinafsi na mchoyo mno wa kutoa pasi.

    Inadaiwa kauli hiyo ya Lewandowski imemchukiza Robben na amemtaka kocha Pep Guardiola ampange mara kwa mara kikosini ama atimke klabuni hapo na kutafuta maisha kwingine.





    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: BIFU KALI:ROBBEN KUTUA MAN UNITED MWEZI JANUARI KISA LEWANDOWSKI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top