Addis Ababa,Ethiopia.
Timu ya taifa ya Tanzania Bara "Kilimanjaro Stars" imeanza vyema michuano ya Cecafa Chalenji Cup baada ya mchana wa leo kuibamiza timu kibonde ya Somalia kwa jumla ya mabao 4-0 katika mchezo wa kundi A uliopigwa katika dimba la Addis Ababa.
Magoli ya Kilimanjaro Stars yamefungwa na John Bocco dakika za 12 na 54 huku mshambuliaji aliye katika kiwango bora kwasasa Elias Maguli naye akifunga dakika za 17 na 66.
Kufuatia ushindi huo Kilimanjaro Stars imefanikiwa kukalia kiti cha uongozi wa kundi A na kuishusha Rwanda ambayo jana iliwafungwa wenyeji Ethiopia kwa bao 1-0.
0 comments:
Post a Comment