728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, November 17, 2015

    TETESI ZA USAJILI ULAYA:COSTA NJE GRIEZMANN NDANI CHELSEA,PEDRO AOMBA KURUDI HISPANIA,MAN CITY YAMGEUKIA DEMBELE

    Tetesi na Paul Manjale


    Griezmann:Chelsea imeripotiwa kufikiria kumtoa mshambuliaji wake Diego Costa pamoja na kitita cha £24m ili kumsajili nyota wa Atletico Madrid Antoine Griezmann.Chelsea imechoshwa na tabia za Costa hivyo inaona suluhisho pekee ni kumuuza nyota huyo aliyefunga magoli mawili pekee katika michezo kumi ya ligi kuu.

    Austin:Aston Villa imeripotiwa kutenga kitita cha £8m kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa QPR Charlie Austin,26.Aston Villa imemgeukia Austin ili kuongeza makali katika safu yake ya ushambuliaji ambayo imekuwa butu hasa baada ya kuondoka kwa Christian Benteke.

    Pedro:Chelsea inafikiria kukubali ombi la kumuuza winga wake Pedro Rodriguez baada ya nyota huyo wa zamani wa FC Barcelona kudai kuwa hana furaha Stamford Bligde na angependelea kurudi Hispania.(Mundo Derpotivo)

    Batshuayi:Rais wa Marseille Vincent Labrune ameviambia vilabu vyote vinavyotaka kumsajili mshambuliaji wake kinda Michy Batshuayi,22 kuandaa kitita cha €35m (£24.5m) vinginevyo nyota huyo Mbelgiji hataruhusiwa kuondoka klabuni hapo. Batshuayi amefunga magoli 17 katika michezo 39.(Fichajes.net)

    Dembele:Manchester City imeongeza kasi katika mbio za kumnasa winga mahiri wa Rennes Ousmane Dembele.Dembele,18 pia ameripotiwa kuwa katika rada za vilabu vya Chelsea, Borussia Dortmund, Atletico Madrid na Red Bull Salzburg baada ya kuendelea kuonyesha kandanda safi akiwa Ligue 1.(Daily Mail)

    Lavezzi:Juventus inafanya kila jitihada ili kuipiku FC Barcelona katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa PSG Muargentina Ezequiel Lavezzi.Kutoka Tuttosport taarifa zinasema Juventus imepanga kumpa Lavezzi mkataba wa miaka miwili utakaomuwezesha kuvuna mshahara wa £3.5m pamoja na bonasi kibao.(Tuttosport)

    Grujic:Everton imeungana na vilabu vya Chelsea, Manchester United na Manchester City katika mbio za kuisaka saini ya kiungo wa Red Star Belgrade ya Serbia Marko Grujic.Grujic,18 ambaye kiuchezaji anafananishwa na Nemanja Matic amejizolea sifa siku za hivi karibuni baada ya kuiwezesha Serbia kutwaa kombe la dunia la vijana la U-21.(Daily Mail)

    Xhaka:Liverpool inataka kuimarisha safu yake ya kiungo kwa kumsajili kiungo matata wa Borussia
    Monchengladbach Mswisi Granit Xhaka mwenye thamani ya £21m.Mbali ya Liverpool,Arsenal imeripotiwa kutuma maskauti wake kumfuatilia kwa karibu kiungo huyo anayetumia vyema mguu wa kushoto.(Bild)

    Silva:Besktasi imeanza kupata ugumu katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa Corinthians,Malcom Silva baada ya Arsenal nayo kuripotiwa kuanza kumfukuzia nyota huyo tegemeo la kikosi cha U-20 cha Brazil.Corinthians iko tayari kumuuza Silva kwa kitita cha £20m.(Mirror)

    Benzema:Real Madrid imedaiwa kuwa itamtupia virago mshambuliaji wake Karim Benzema ikiwa nyota huyo Mfaransa atakutwa na hatia katika kesi ya kutaka kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu katika kashfa ya mkanda wa ngono inayomuhusisha kiungo wa Lyon,Mathieu Valbuena.(AS)

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: TETESI ZA USAJILI ULAYA:COSTA NJE GRIEZMANN NDANI CHELSEA,PEDRO AOMBA KURUDI HISPANIA,MAN CITY YAMGEUKIA DEMBELE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top