Hatimaye Chelsea ikiwa Stamford Blidge imeamka toka katika usingizi wa kupata matokeo mabovu baada ya jioni ya leo kuilaza Norwich City kwa bao 1-0.
Goli pekee la mchezo huo limefungwa kipindi cha pili na mshambuliaji Diego Costa.Katika mchezo mwingine Arsenal imepokea kipigo cha magoli 2-1 toka kwa West Bromwich Albion katika mchezo uliopigwa katika dimba la Hawthorns.
West Brom imepata magoli yake kupitia kwa James Morrison na Mikel Arteta aliyejifunga akijaribu kuzuia krosi ya James McClean,goli la Arsenal limefungwa na Olivier Giroud.
Matokeo mengine:Leceister City imeifunga Newcastle United kwa magoli 3-0 na kuongoza ligi baada ya kujikusanyia pointi 28,Everton 4-0,Swansea City 2-2 Bournemouth,Southampton 0-1 Stoke City.
0 comments:
Post a Comment