Cairo,Misri.
NYOTA wa zamani wa Zamalek Amr Zaki amefichua siri iliyofanya ashindwe kujiunga na Real Madrid licha ya miamba hiyo ya Hispania kuonyesha nia ya kutaka kumsajili.
Zaki ambaye kwa sasa ameachana na soka baada ya kutamba na timu ya taifa ya Misri,Zamalek na kisha Wigan kwa mkopo amekiambia kituo cha luninga cha Dream kama siyo tamaa za viongozi wa Zamalek angechezea Real Madrid ama Liverpool kwani alipata ofa nyingi sana baada ya kuifungia Wigan goli za kutosha msimu wa mwaka 2008-2009.
Amesema "Wakati niko Wigan nilipata ofa nyingi sana kutoka vilabu vya Real Madrid,Liverpool na hata vile vya Italia navyo vilinitaka.
"Sababu ya vilabu vyote hivyo kunitaka ilikuwa ni magoli ambayo tayari nilikuwa nimeifungia Wigan.Nakumbuka wakati huo nilikuwa naongoza kwa ufungaji huku nikiwa nimevifunga vilabu kama Westham United na Liverpool.
Bodi ya Zamalek iliyokuwa ikiongozwa na Mamdouh Abbas ilipopata habari hizo ikaweka ngumu kwa kukataa paundi millioni 15 za Uingereza na kutaka paundi milioni 250 za Misri"
"Kisha nikamuuliza Abbas paundi milioni 250?Unamuuza Messi?Akajibu hapana ila we we ni zaidi ya Messi"
0 comments:
Post a Comment